Isaiah 24:7-12

7 aDivai mpya inakauka na mzabibu unanyauka,
watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.
8 bFuraha ya matoazi imekoma,
kelele za wenye furaha zimekoma,
shangwe za kinubi zimenyamaza.
9 cHawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo,
kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.
10 dMji ulioharibiwa umekuwa ukiwa,
mlango wa kila nyumba umefungwa.
11 eBarabarani wanalilia kupata mvinyo,
furaha yote imegeuka kuwa majonzi,
furaha yote imefukuziwa mbali na dunia.
12 fMji umeachwa katika uharibifu,
lango lake limevunjwa vipande.
Copyright information for SwhNEN